Spika wa seneti, Amason Kingi,amewataka magavana nchini kutokuwa na uoga wanapofika mbele ya seneti, bali washirikiane kwa uwazi katika kueleza matumizi ya fedha za ugatuzi.
Akiwa mjini Busia baada ya kukutana na gavana Paul Otuoma, Kingi amesema seneti haina nia ya kuwatimua magavana, bali kuhakikisha uwajibikaji.
Aidha, amepinga madai ya kuwepo kwa uhasama kati ya maseneta na magavana, na kuwataka viongozi wa kaunti kuchukua hatua dhidi ya maafisa wao wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi.