Watu wanne wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kapenguria baada ya kupatika wakiwa wamemchinja punda, katika mtaa wa Eastleigh eneo bunge la Kapenguria kaunti ya Pokot Magharibi hali ambayo imezua hofu miongoni mwa wakaazi eneo hili kuhusiana na nyama iayouzwa mjini

Aidha wakazi wameitaka Idara husika kufanya uchunguzi iwapo nyama zinazouzwa ni salama.