Kamati za amani kutoka mataifa ya Kenya na Uganda zimekubaliana kwa kauli moja kuwakamata wahalifu na kuwawasilisha katika asasi za kiserikali.

Hatua hiyo kulingana na kamati hizo,itasaidia kupambana na majangili ambao wamekuwa wakiyumbisha usalama baina ya mataifa hayo mawili.

Wakuzungumza eneo la Kosike katika wilaya ya Amudat nchini Uganda,viongozi hao wakiwemo vijana na machifu kutoka Kenya na Uganda wametangaza kwamba,wahalifu wote kwenye mipaka hiyo watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Wakiongozwa na chifu wa Kalapata kutoka Pokot Kaskazini Julius Kaliyamoi,amesema,wamebuni makundi ya watu 10 kutoka kila lokesheni ambayo itatumika kutoa ripoti kwa idara ya polisi kwa muda ufao.

Kwa upande wake mkuu wa usalama kiwango cha LC3 nchini Uganda Logoree Elijah ametangaza kwamba,watabuni miungano ya amani kati ya kenya na Uganda ili kusaidia katika kurejesha utulivu na amani mpakani humo.

Aidha,amependekeza kwamba,kila muuzaji wa mifugo apate stakabadhi za kuonyesha amenunua mifugo hiyo ili kuziba mwanya wa wizi wa mifugo kwenye mpaka huo.