Wafanyibiashara mjini Kitale, wameikosoa serikali ya kaunti hiyo kwa madai ya kupuuza katiba, hususan kuhusu kipengele cha kushirikisha umma, kabla ya kuutekeleza sera au sheria yeyote,mfano ni ilani ya siku 7 ya kutaka wafanyi biashara wa vibanda kuvibomoa na la sivyo vibomolewe kwa lazima,

Kulingana na mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara na viwanda, tawi la kaunti hiyo Titus Kilong’i, ameitaja hatua hiyo kuwa isiyofaa na inayofanywa kwa pupa, ikizingatiwa kuwa masoko yakiwemo Masinde Muliro Complex, la zaidi ya kima cha shilingi milioni mia nane na lile la Railway la kima cha zaidi ya shilingi milioni moja, haijakamilika kufikia sasa.