Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE umeanza rasmi hii leo.

Baraza la kitaifa linalosimamia mitihani KNEC limesema,shuguli zote zilikamika jinsi ilivyokuwa imeratibiwa kupisha mitihani hiyo kuanza.

Watahiniwa wataanza kwa kukalia mitihani ya lugha ya kifaransa,kijerumani,Arabik na lugha ya ishara.

Mkurugenzi mtendandaji wa KNEC Davind Njengere amebainisha kwamba,jumla ya watahiniwa 996,078 watakalia mtihani huo mwaka huu.

Watahiniwa wengine wapatao 1,298,089 watakalia mtihani wa KPSEA ambayo itaanza rasmi wiki kesho huku wengine 1,130,669 wakifanya mtihani wa KJSEA.

Aidha,Njengere amesema kwamba,vituo vya kuhifadhi mitahani hiyo imeongezwa kutoka 617 mwaka jana hadi 642 kurahisisha usafirishaji wa mitahani hiyo hadi vituo vya kufanyia mitihani yenyewe.