Kutokana na ongezeko la visa vya utovu wa usalama mpakani mwa kaunti ya Pokot Magharibi na Turkana Wito umetolewa kwa wakazi kuishi kwa amani na utangamano.
Akizungumza na wanahabari mbunge wa Sigor Peter Lochakapong amewataka wenyeji kufanya biashara zao bila kuwepo kwa mizozano akisema kwamba ni jukumu la asasi za usalama kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria akikashifu vikali ripoti kwamba kuna baadhi ya maafisa wa NPR ambao badala ya kuwalinda raia na mali zao wamejitwika jukumu la kuwalinda wawekezaji wanaoendesha biashara zao katika eneo hilo
Mbunge huyo amesema kwamba kuwepo kwa amani italeta maendeleo akiwataka maafisa wa usalama kulinda mali ya wananchi na kudumisha utulivu.