Watu 21 wameripotiwa kufariki kutokana na mapropomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa katika eneo la Chesongoch katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen aliyezuru eneo hilo siku ya Jumamosi alisema kuwa watu wengine 30 hawajulikani waliko na wengine 25 wakijeruhiwa.

Shirika la Msalaba Mwendundu limesema majeruhi wengine 21 walibebwa kwa ndege ya kijeshi kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret kwa matibabu zaidi.

Shuguli za kutafuta miili zaidi inatarajiwa kuendelea leo Jumapili wakati vikosi vya usalama vikitumwa eneo hilo kushirikiana na wananchi kutafuta miili hiyo.

Gavana wa kaunti hiyo Wisley Rotich ametangaza kwamba,zoezi la kuwatafuta wanaohofiwa kufunikwa kwenye vifusi hivyo litaendelea leo.

Kulingana naye,kila mwenye nia njema aliyehitumu umri wa miaka 18 na anayetaka kujihusiha kwenye zoezi hilo watakutana eneo la St Maurus kabla ya zoezi hilo kung’oa nanga mwendo wa saa mbili asubuhi.