Mgogoro mpya umezuka kati ya serikali na waahadhiri wa vyuo vikuu UASU, kutokana na kucheleweshwa kwa kutiwa saini na kutekelezwa kwa mkataba wa maelewano ya pamoja CBA, vilevile madai ya UASU kwamba serikali inavuruga mchakato wa kuwaajiri wafanyikazi katika chuo kikuu cha nairobi.

Chama hicho sasa inaonya kwamba iwapo maswala hayo hayatashughulikiwa huenda waahadhiri na wafanyikazi wakaanza mgomo, hali inayoweza kusababisha kuyumba upya kwa shughuli za elimu katika chuo kikuu cha Nairobi.

Mzozo huu unajiri miezi michache tu baada ya baraza jipya kuteliwa, ili kurejesha utulivu kufuatia msukosuko wa muda mrefu wa uwongozi.

Akizungumza katika chuo kikuu cha Nairobi, katibu mkuu DKT Maloba Wekesa, ameilaumu serikali na uongozi wa chuo, kwa kukiuka mkataba wa CBA, kati ya mwaka 2021-2025.