Kama njia moja ya kuepuka mizozo ya mara kwa mara ni sharti jamii na viongozi kuhusishwa kikamilifu wakati madini inapopatikana.
Akizungumza alipohudhuria hafla ya mchango wa kanisa ya dini ya Roho Mafuta Pole Afrika katika eneo la Sook kaunti ya Pokot Magharibi kiongozi wa wengi kwenye bunge la seneti aliye pia seneta wa kaunti ya Kericho Aaron Cheruiyot amesema kwamba ukusanyaji wa maoni na kuihusisha jamii unasaidia kuepuka mizozo baina ya jamii mbalimbali na hata baadhi wakitaka kuongeza mipaka yao ili kunufaika na madini hayo.
Wakati huo Seneta Cheruiyot ametoa wito wa ushirikiano baina ya viongozi kutoka kaunti ya Pokot Magharibi, Turkana na Elgeyo Marakwet katika kutafuta Suluhu kuhusiana na visa vya utovu wa usalama maeneo ya mipakani .