Rais William Ruto ameagiza kuanzishwa kwa Mpango wa Kitaifa wa Udhamini wa Ksh.500 milioni ili kusaidia jamii za walio wachache kupata elimu bora.
Akizungumza wakati wa siku ya kimataifa ya haki za walio wachache katika Ikulu ya Rais , Rais Ruto amebainisha kuwa mpango huo, kwa ushirikiano na wahusika binafsi, utawasaidia watoto kutoka jamii za walio wachache ,maskini na zilizotengwa kupata elimu ya sekondari na ya juu.
Vile vile, amebainisha kuwa Wizara ya Elimu itatenga Ksh.200 milioni kila mwaka ili kuboresha Miundombinu ya Elimu, na kuvipa shule na vyuo vikuu katika maeneo yaliyotengwa ili uwezo wa kujisimamia .
Pia ameagiza Wizara ya Maji, Barabara, Afya pamoja na hazina ya kitaifa ya usawazishaji kuweka kipaumbele maeneo ya wachache na yaliyotengwa ili kutoa maji safi, Barabara, na vituo vya afya ili kuboresha maisha ya jamii hizo.