Serikali imeibua wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa visa vya ulaghai wa mishahara na ubadhirifu ndani ya Sekta ya utumishi wa umma, ikionya kwamba hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya maafisa wanaohusika katika vitendo hivyo.

Akizungumza katika Ukumbi wa Maonyesho wa Nairobi, Jamhuri Park, waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku amesema baadhi ya maafisa wamekuwa wakishirikiana na watumishi wa umma kubadilisha makundi ya kazi bila idhini sahihi kutoka kwa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC), na kusababisha hasara za kifedha.