Serikali yatenga Shilingi milioni 29 kusaidia waathiriwa wa mafuriko katika Kaunti ya Trans Nzoia, Waziri wa Mazingira Deborah Barasa amesema angalau familia 3,400 zimelazimika kuhama makazi na zaidi ya watu 20,000 wameathiriwa.

Aidha Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, idara ya utabiri wa hali ya anga imebainisha kuwa mvua inazoendelea za Oktoba-Novemba-Desemba (OND) 2025 zimesababisha kujaa kwa udongo na mafuriko , hasa katika nyanda za juu magharibi na maeneo ya Bonde la Ufa.

Idara ilitoa rambirambi kwa familia zilizoathiriwa na maporomoko ya ardhi hivi karibuni huko Chesongoch, Kaunti Ndogo ya Marakwet Mashariki.