Huku kenya ikiungana na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya ishara, madktari na maafisa wa watu wenye ulemavu katika kaunti ya transnzoia, wameihamasisha umma kuhusu jinsi watu hupoteza uwezo wao wa kusikia.
Daktari Francis Barchebo na Bernard Masioge ambaye ni afisa wa maswala ya watu wenye ulemavu , wametoa wito kwa wakenya kutokuwa na mazoea ya kusikiliza msiki kwa sauti ya juu waieleza kuhusu hatari zake, kwani ni mojawapo ya sababu kuu ya matatizo ya kusikia hasa miongoni mwa vijana.