Tume ya Utawala wa haki, maarufu kama Ofisi ya Ombudsman, imefungua rasmi ofisi mpya na kubwa zaidi jijini Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, kwa lengo la kuwahudumia wakazi wa eneo lote la Kaskazini mwa bonde la ufa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa tume hiyo Charles Dulo amesema kazi imeanza rasmi na maafisa watakuwa tayari kuanzia kesho kupokea na kushughulikia malalamishi ya wananchi, akiwahimiza kujitokeza na kutoa kesi zao bila hofu.

Naibu Gavana wa Uasin Gishu Evans Kapkea ameahidi ushirikiano kamili wa serikali ya kaunti kwa Ombudsman, huku akiwataka wakazi wa North Rift kutumia ofisi hiyo kuripoti dhuluma, matumizi mabaya ya mamlaka na ucheleweshaji wa huduma katika taasisi za umma.
Naye mwanaharakati wa haki za binadamu Kimtai Kurui amesema Ombudsman imewasaidia wananchi wengi na husikiliza malalamishi yao na kuyafuatilia hadi haki inapotendeka.