Katika hatua za kupunguza idadi ya vijana wanaokabiliwa na matatizo ya afya ya akili Shirika la Afya care foundation kwa ushirikiano na Hospitali ya Tiwani limeandaa kongomamano kwa vijana eneo bunge la endebess kaunti ya Trans Nzoia ili kutoa hamasa kama njia moja ya kukabiliana na tatizo hilo.
Shirika hilo ambalo hutoa huduma kwa vijana walio na umri wa kati ya miaka 13 hadi 35 katika kaunti saba ikiwemo Pokot Magharibi,Trans Nzoia,Kakamega,Bungoma,Vihiga,Turkana na Busia, Culistus Wekesa mkurugenzi wa shirika hilo amesema kwamba idadi kubwa ya visa vinayochangia vijana kukumbwa na msongo wa mawazo ni ukosefu wa ajira na matumizi ya dawa za kulevya.
Hafla hiyo imefanyika kwenye shule ya upili ya wasichana ya sabwani ambayo ilihudhuriwa na mamia ya vijana ambao walieleza kunufaika na mafunzo hayo.