Viongozi wanaoegemea mrengo wa serikali wamemsuta vikali aliyekuwa naibu rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua wakimtaja kama kiongozi asiyekuwa na maono yoyote kwa wakenya.
Viongozi hao wamesema,serikali ya rais William Ruto inaendeleza kutimiza ahadi kwa wakenya wakiwataka wakazi wa Pokot Magharibi kumuunga mkono kiongozi wa taifa katika azma yake ya kurejea ikulu kwa muhula wa pili mwaka wa 2027.

Wakizungumza wakati wa hafla ya kuwawezesha akina mama katika kaunti hiyo katika mji wa Makutano eneo bunge la Kapenguria,viongozi hao wamesema,uchumi umeanza kuimarika na kwamba,serikali ya kenya kwanza iko imara kuboresha maisha ya wananchi
Wakiongozwa na msaidizi wa rais Faruok Kibet,viongozi hao wamekejeli matamshi ya upinzani wanaokosoa uongozi wa nchi wakisema,hawana jawabu kwa matatizo yanayowakibili wananchi.
Mkutano huo unahudhuriwa na spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula,mbunge wa kapenguria Samuel Moroto,Mbunge wa Sigor Peter Lochakapong,kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Aaron Cheruiyot,mbunge mwakilishi wa akina mama wa pokot magharibi Rael Kasiwai miongoni mwa wengine
