Na Ivy Omwenga
Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Moi mjini Eldoret wameungana na wenzao kote nchini katika mgomo wa kitaifa wa wahadhiri unaoendelea.
Viongozi wa Chama cha wahadhiri wa chuo hicho,walikutana chuoni Eldoret na kutangaza kwamba,kamwe hawatarejea darasani hadi serikali itakapotimiza makubaliano ya kazi CBA ya mwaka 2021-2025.
Wakiongozwa na katibu mkuu wa tawi hilo, Dkt. Busolo Wekesa, wahadhiri hao wanasema wamechoshwa na ahadi za uongo kutoka kwa serikali na kusisitiza kwamba,ni sharti shilingi bilioni 2.5 zilipwe kabla yao kurejea darasani.
Naye mwenyekiti wa wahadhiri hao Richard Okero anadai kuwa, wahadhiri wamekuwa wakistaafu bila ya kupewa pensheni zao jambo alilolitaja kama hujma.
Hali hii imesamabaratisha shuguli za masomo chuoni humo huku wanafunzi wakisalia njia panda.Wahadhiri hao wamenasisitiza kuwa,mgomo utaendelea kila siku hadi pale serikali itakapowalipa fedha zao.