Huku tume huru ya uchaguzi na mipaka  IEBC inapoendelea na zoezi la usajili wa wapiga kote nchini, afisa anayesimamia tume hiyo kaunti ya Trans Nzoia Patrick Wanyama, amewahimiza wakaazi ambao bado hawajajisajili kujitokeza kwa wingi ili wasajiliwe kama wapiga kura kwenye uchaguzi ujao wa mwaka wa 2027.

Akizungumza afisini mwake mjini Kitale Kaunti ya Trans Nzoia Wanyama amewataka vijana hasa wa kizazi cha GEN -Z kujisajili kwani wana uwezo mkubwa wa kuwateua na kubadilisha viongozi wanaowahitaji.

Kadhalika Wanyama amewahimiza waakazi wa kaunti ya Trans Nzoia na Kenya kwa jumla kudumisha amani na utangamano.