Wakazi wa kaunti ya Pokot Magharibi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kutoa maoni na mapendekezo yao kwenye sekta mablimbali kama hatua moja ya kuboresha huduma kwa wanachi kwenye bajeti ya mwaka wa 2026 2027
Akizungumza na wanahabari katika eneo la Kishaunet waziri wa fedha kaunti ya Pokot Magharibi Paul Woyakapel amesema vikao hivi ni muhimu katika kufahamu ni nini hasa wananchi wangeitaka serikali kutekeleza
Wakati huo uo waziri huyo ametoa wito kwa wenyeji wa kaunti hii kujitokeza kwa wingi tarehe 12 na 13 kuhudhuria hafla ya ukusanyaji maoni ya umma kwenye wadi zote 20 ili kuangazia mapendekezo yao kwenya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2026|2027.