Wakaazi wa Keringet katika wadi ya Mnagei eneobunge la Kapenguria katika kaunti ya Pokot Magahribi, wamepinga vikali hatua ya kuhamishwa kwa sehemu ya chuo kikuu hadi sehemu tofauti.
Wakizungumza na Aperit fm kule Keringet wamesisitiza kuwa hamna haja ya serikali kutafuta sehemu nyingine ilihali kuna jengo lililoko eneo hilo iliyo gharimu mamilioni ya fedha, wameirai serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi, kuhakikisha chuo hicho kinasalia katika maeneo hayo.
Wakaazi hao wakiongozwa na Alex Kiptoo wamesema hali hiyo itachangia ukuaji wa uchumi katika eneo hilo huku wakiwataka wanasiasa kujitenga na swala la urejesho wa chuo hicho, huku wakitoa wito kwa Rais William Ruto kuingilia kati na kutafuta suluhu.