Wakaazi wa eneo la Ywalateke katika wadi ya Chepareria kaunti ya Pokot Magharibi,wanaitaka serikali ya kaunti hiyo kukarabati barabara ya Kapkatanyang kuelekea Kayemit wakisema,ubovu wake umetatiza shuguli za usafiri.
Wakiongozwa na Jacob Aramtori,wakazi hao wanadai kuwa,hali mbovu ya barabara hiyo imesalia kuwa kero kwa miaka mingi na kwamba kuna haja ya kukarabatiwa ili kurahisisha shuguli za uchukuzi.
Aidha,wametoa wito wa kujengwa vivukio kwenye mito katika eneo hilo wakisema,kila mvua inaponyesha,wakazi wanaoshi kwa hofu ya kusombwa na mafuriko