Wakaazi katika eneo la Pokot ya Kati kaunti ya Pokot Magharibi wametakiwa kusalimisha bunduki haramu wanazozimiliki kinyume cha sheria kabla ya serikali kuanza kutumia nguvu kuzitwaa.

Kwa mujibu wa kamishina msaidizi wa eneo la Chesegon Peter Njuguna,serikali itawasemehe wote watakaorejesha bunduki zao kwa hiari na kwamba,serikali itawaadhibu watakaokaidi agizo lilitolewa la kusalimisha silaha haramu.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya kipekee,Njuguna amesema kwamba,serikali itatumia mwezi huu wa septemba wa msamaha kwa wote wataosalimisha bunduki zao.

Aidha,amesema,watakaosalimisha bunduki zao watapokea mafunzo na usaidizi kutoka kwa serikali ili kuendeleza maisha yao kupitia msaada huo.

Kamishna huyo ameeleza kwamba,juhudi hizo zinanuia kurejesha amani katika eneo pana la Pokot ya Kati

Wakati huo huo,kamishna Njuguna ameeleza nia ya kuwapatiNISHA wakaazi kutoka kaunti ya Pokot Magharibi na wenzao kutoka kaunti ya Elgeyo Marakwet ambao wamekuw awakihasimiana kwa muda mrefu.