Wakazi katika eneo bunge la Kapsaret kaunti ya Uasin Gishu wameandamana wakimtaka mbunge wao Oscar Sudi ajiuzulu kwa kutelekeza miradi ya maendeleo.
Wakizungumza na wanahabari,wakazi hao wanadai,mbunge huyo amekuwa akitumia nguvu dhidi ya wakazi wanaopinga uongozi wake.

Idadi kubwa ya waandamanaji imedai kuwa,wamekuwa wakipokea vitisho kila mara wanapouliza maswali kuhusu uongozi wa mbunge huyo.
Hata hivyo,wazee wa jamii hiyo wametoa wito kwa serikali kuanzisha uchunguzi dhidi ya madai yaliyoibuliwa na kuwataka wananchi kuwa na subra wakati lalama zao zinaposhuguliwa.
