Mahafala 2,260 kutoka kambi za wakimbizi za Kakuma na Kalobeyei, kaunti ya Turkana, wamehitimu kama wataalamu wa teknolojia ya mtandao baada ya kukamilisha mafunzo maalum katika chuo cha ufundi cha Don Bosco Kakuma.

Ujuzi waliopata kutokana na mafunzo hayo utawawezesha kiuchumi na kutatua b aadhi ya changamoto wanazokumbana nazo kutokana na hali yao ya kutengwa kama wakimbizi.

Wakati wa sherehe za kufuzu, afisa mkuu wa shirika la emobes, mwenda, alieleza kuwa mafunzo hayo yamefungua milango mipya kwa vijana na watu wazima katika kambi hizo, kuwapa maarifa yatakayowasaidia kupata ajira na kuboresha maisha yao katika siku zijazo.

Mradi huu unalenga kupanua nafasi kwa wakimbizi kushiriki kikamilifu katika fursa za kidijitali zinazokua kwa kasi nchini na duniani kote.