Wakulima wa eneo la Moiben katika kaunti ya Uasin Gishu wameanza kugeukia teknolijia kama njia mojawapo ya kuboresha uzalishaji wa chakula kwenye kaunti hiyo.

Wakulima hao kwa sasa wanapokea mafunzo ya namna ya kutumia teknoljia katika kilimo chao katika eneo hilo ambalo limekuwa nguzo katika uzalishaji wa chakula nchini.

Katika maonyesho ya kilimo yanayoendelea eneo la Moiben,ubunifu mkubwa umejitokeza miogoni mwa wakulima hao ikiwemo matumizi ya droni ya kunyunyiza dawa na mbolea shambani.

Wengi wa wakulima wanaohudhuria maonyesho hayo,wametaja uvumbuzi huo kama wenye tija wakieleza kwamba,utaharakisha shuguli za shambani na kupunguza gharama za ukulima