Walimu wa shule za sekondari msingi JSS wametishia kugoma mwezi Januari mwaka ujao iwapo serikali itafeli kuwaaajiri katika mkataba wa kudumu.

Muungano wa kutetea maslahi ya walimu wa shule za sekondari na vyuo vya kadri KUPPET,umepinga mapendekezo ya rais ya kuwaajiri walimu wa JSS kwa kandarasi za miaka miwili.

Katika kikao na wanahabari mjini Makutano kaunti ya Pokot Magharibi,katibu mkuu wa KUPPET kaunti hiyo Alfred Kamuto amesema,walimu wa JSS wamekuwa wakifanya kazi kubwa na kupokea fedha zisizotosha.

Viongozi wa KUPPET wametaka serikali kuwapa uhuru walimu wa JSS kuwa na usimamizi wao badala ya kuwa chini ya shule za msingi.

Kulingana na mwenyekiti wa KUPPET kaunti hiyo Joel Todokori,serikali inafaa kuwapa walimu hao mkataba wa kudumu la sivyo,watashiriki mgomo mwaka ujao.

Kaaunti ya Pokot Magharibi ina jumla ya walimu 400 wa JSS ambao vilevile wanashinikiza kuajiriwa katika mkataba wa kudumu