Waziri mkuu wa zamani marehemu Raila Odinga ametuzwa tuzo ya hali ya juu nchini, kama chief of the order of the golden heart (c.g.h), heshima kuu zaidi nchini kenya.

Heshima hiyo ilitolewa na rais william ruto wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa.

Notisi ya gazeti la serikali ya tarehe 20 oktoba 2025, imethibitisha kutunukiwa heshima ya daraja la kwanza c.g.h kwa raila, ikimtambua kwa mfano wa ujasiri, uvumilivu, , kujitolea kwa dhati kwa maadili ya demokrasia na utawala bora, na huduma ya uaminifu kwa wananchi.