Mgomo wa wahadhiri katika vyuo vikuu vya umma bado unaendelea, huku wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Moi wakisisitiza kuwa hawatarudi darasani hadi serikali itimize matakwa yao kikamilifu Wakisema serikali imekosa kujali masuala yao ya mishahara, marupurupu, na mazingira bora ya kazi.

Kwa upande wao Wanafunzi wanasema masomo imekwama licha ya kulipa karo, jambo linaloweza kuchelewesha kuhitimu kwao.

Wahadhiri wanaitaka serikali kuchukua hatua za haraka kumaliza mgomo huo ili masomo yarudi katika hali ya kawaida.