Huku taifa likiadhimisha siku ya mazingiria wito unazidi kutolewa kwa wananchi kupanda miti kwa wingi katika hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Akizungumza katika shule ya msingi ya Kapsangar wadi ya Tapach kaunti ya Pokot Magharibi wakati wa hafla ya upanzi wa miti katibu mkuu wa kazi za umma Joel Arumonyang ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kupanda miti angalau thelathini ili kuhakikisha taifa linadhibiti ukataji wa miti na kutunza mazingira
Kadhalika katibu Arumonyang ametoa wito kwa taasisi za elimu kutumia mbinu salama za kupika kama mojawapo ya mikakati ya kudhibiti uchomaji wa makaa katika eneo hili