Wenyeji wa Kaunti ya Bungoma wameshauriwa kuwalea wazee katika mazingira bora.

Ni wito wake gavana wa kaunti ya Bungoma Ken Lusaka akizungumza katika eneo la Musese wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wazee,ambapo amesema wana haki ya kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo afya  akiongeza kuwa wazee hutekeleza wajibu mkubwa katika jamii.

Kwa upande wake mbunge wa Kimilili Didimas Barasa ametaka mpango wa serikali wa inua jamii kufanyiwa marekibisho huku mwakilishi wa kina mama kaunti ya Bungoma Catherine Wambilianga akiitaka serikali kuendeleza mpango wa kuandikisha wazee kwa bima ya afya ya sha.