Katibu mkuu wa muungano wa walimu wa shule za upili, KUPPET, Akelo Misori, amekosoa vikali hatua ya wizara ya elimu kupeleka walimu kufundisha katika shule za sekondari msingi, maarufu kama jss, hasa maeneo ya mashinani.
Misori amesema walimu na wanafunzi wamepoteza mwelekeo wa mafunzo kutokana na tofauti kubwa za mazingira kati ya mijini na mashinani.
Aidha, Misori ametilia shaka utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu, akidai kuwa ulianzishwa bila maandalizi madhubuti wala mikakati ya kutosha.