Wizara ya Elimu inakamilisha muundo mpya wa ada ya shule kwa shule ya upili kabla ya mabadiliko ya 2026, wakati wanafunzi wa gredi ya 9 watahamia gredi ya 10 chini ya Mtaala unaozingatia Umahiri (CBC).
Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari William Sugut amesema kuwa wakuu wa shule na maafisa wa wizara kwa sasa wanafanya kazi ya kuandaa mfumo wa ada iliyorekebishwa.
Kauli ya Sugut inajiri wakati Kenya inajitayarisha kuhamia kikamilifu kwa mpito wa kwanza CBC.
Chini ya mfumo huo mpya, wanafunzi wa shule za upili, gredi ya 10-12, watafundishwa ujuzi unaoendana na elimu ya vipaji.