Viongozi na vijana katika eneo la Murkwijit katika kaunti hii ya Pokot Magharibi,wamewatolea mwito vijana kutotumika na wanasiasa kuvuruga amani ya wakaazi.
Kauli yao inajiri siku chache kufuatia tukio ambapo,vijana waliokuwa wamejihami kwa silaha butu walivamia kanisa la Full Gospel eneo la Murkwijit na kusambaratisha shuguli ya uchangishaji wa fedha kanisani humo.
Tukio hilo lilifuatia kuwepo kwa wanasiasa wa marengo miwili mikubwa katika kaunti hiyo ya Message na Network kwenye hafla hiyo.
Kulingana na kiongozi wa vijana eneo hilo Musa Ndiaye,vijana wanastahili kujiepusha na wanasiasa wachochezi amba onia ya oni kuwagonganisha wakaazi kwa faida zao za kibinafsi.