Na Ivy Omwenga

Viongozi wa dini ya kiislamu kutoka eneo la kaskazni mwa bonde la ufa wamepongeza hatua ya Bunge la kitaifa kuchunguza mzozo wa uongozi ndani ya Baraza Kuu la Waislamu nchini, SUPKEM.

Ombi hilo limewasilishwa na Jamal Diriwo Omari kutoka Kaunti ya Uasin Gishu, anayedai kuwa uongozi wa sasa chini ya Al-Hajj Hassan hauna uwazi na unakiuka kanuni za baraza.

Bunge litawasilisha ombi hilo kwa Kamati ya Sheria na Haki za Kibinadamu ili kuchunguza, huku likisisitiza kuwa masuala ya dini hayawezi kuingiliwa moja kwa moja na serikali.

Kulingana na kiongozi mwingine wa kidini Asman Koskei,ni kuwa hatua hiyo inaleta matumaini mapya ya kurejesha umoja na uwajibikaji ndani ya SUPKEM baada ya miaka mingi ya migogoro ya uongozi.