Baadhi ya viongozi wa upinzani, sasa wanaitaka tume ya uwiano na utengamano wa kitaifa NCIC, kuwachukulia hatua kali viongozi walioeneza jumbe za ukabila baada ya matamshi ya gavana wa nyeri mutahi kahiga, kuhusu kifo cha aliyekuwa waziri mkuu raila odinga.
Viongozi hao wakiongozwa na aliyekuwa mbunge wa Mukuruweini kabando wa kabando, wanasema mbunge wa dadab farah mahalim, dan wanyama wa webuye magharibi na gavana wa homabay gladys wanga, wanapaswa kuandamwa na mkono wa sheria.
Kadhalika wameikashifu NCIC, kwa kuegemea upande mmoja kwa kumuandama mutahi kahiga pekee aliyeonekana kudhihaki kifo cha raila odinga.