Katibu katika wizara ya fedha Chris Kiptoo ametangaza kwamba uchumi wa Kenya uliimarika mwaka wa 2025, huku mfumuko wa bei ukipunguza mzigo kwa wakenya kupitia kupungua kwa bei ya bidhaa.

Katika taarifa kwa umma Kiptoo ameangazia maendeleo yaliyopatikana katika kuimarishwa kwa uchumi huku akikiri kwamba bado kuna kazi zaidi ya kuboresha viwango vya mapato ya Wakenya.

Kiptoo amesisitiza azma ya serikali kuboresha pato la Wakenya kwa kiasi kikubwa, akifichua kwamba msukumo wa Kenya kuwa uchumi wa kipato cha juu uliegemezwa katika kuongeza pato la kila mtu.