You are currently viewing MDHIBITI WA BAJETI AMEONYA KUWA BILI YA SHILINGI BILIONI 524.8 AMBAZO HAZIJALIPWA ZINADUMAZA UCHUMI

MDHIBITI WA BAJETI AMEONYA KUWA BILI YA SHILINGI BILIONI 524.8 AMBAZO HAZIJALIPWA ZINADUMAZA UCHUMI

Bajeti ya maendeleo ya serikali ya kitaifa inafikia Shilingi bilioni 612.98, kumaanisha bili ambazo hazijalipwa sasa karibu inamaliza mgao wote wa serikali.
Mdhibiti wa bajeti ya serikali Magret Nyakango amesisitiza kuwa malimbikizo haya yanafikia aina fiche ya deni la umma ambalo linazidi kuzorotesha biashara ndogo na za kati (SMEs) ambazo zinategemea malipo ya haraka ya serikali ili kuendelea kufanya kazi.

Aidha Nyakango amesema bili zinazosubiri kulipwa na wizara, idara na mashirika ya serikali ya kitaifa (MDAs) zimepanda hadi Sh524.84 bilioni.
Nyakang’o sasa anaonya kwamba serikali “inazama katika deni, katika bili zinazosubiri,” na ni athari mbaya kwa uchumi.