Waumini wa dini ya kiislamu kote nchini wameungana na wenzao leo hii kusherehekea sikukuu ya idd ul-fitr.

Idd husherehekewa kuashiria mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan, kwa kawaida waumini wengi wamekuwa wakisherehekea kwa kuwaalika watu wasiojiweza katika jamii kuungana nao katika sherehe hizo.

Sherehe hii inafanyika baada ya waziri wa maswala ya ndani ya nchi kipchumba murkomen, kuchapisha rasmi kwenye gazeti la serikali siku ya leo kuwa likizo ili kutoa nafasi kwa waumini.

Viongozi wa dini ya kiislamu katika mji wa Makutano eneobunge la Kapenguria katika kaunti ya Pokot Magharibi wakiongzwa na Haji Jumbe Omar, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza kuu la waislamu katika kaunti ya Pokot Magharibi, SUPKEM, ametoa wito kwa waislamu wote kusalia watakatifu hata baada ya kumaliza mwezi wa Ramadhan.

Kwa upande wake Abdulkarim Kibwana Sakwa, ambaye pia ni mgombeaji wa kiti cha uwakilishi wadi, katika wadi ya Mnagei Eneo bunge la Kapenguria, amewahimiza wananchi wote wa jamii ya kiislamu na dini ziningine kuishi kwa amani na umoja ili kuindeleza taifa hili kimaadili.

Ameawataka viongozi kuwa makini hata zaidi na matamshi wanayoyatoa hadharani kwenye majukwa ya kisiasa, huku akionya kwamba yanaweza lemaza shughuliza za taifa.

Viongozi hao vilevile wamelikashifu vikali tukio la mashambulizi ya kivita yanayoendelea baina ya mataifa ya marekani, israel na iran katika mwezi mtukufu wa ramadhan.