Wakazi wa eneo la Nakuyen katika wadi ya Suam kaunti ndogo ya Kacheliba,wamewataka viongozi kutoka eneo hilo kuwasaidia katika mchakato wa upatikanaji wa vituo vya afya vya umma.
Katika mazungumzo na kituo hiki,wakazi hao wamelalamikia umbali wa vituo vya afya vya umma kutoka sehemu wanakoishi wakisema,imelemaza huduma muhimu za kiafya.
Aidha,wakazi hao wamedai kuwepo kwa idadi kubwa ya vituo vya afya vya kibinafsi sehemu hiyo ambavyo vinatoa huduma za afya kwa gharama ya juu.
Kulingana nao,vituo vya afya vya umma vya Kacheliba na Pakatusa viko kilomita nyingi kutoka Nakuyen hali ambayo imekuwa ikiwalazimisha wakiokuwa na uwezo wa kifedha kutafuta huduma hizo umbali huo.