Naibu mwenyekiti wa wanabodaboda katika kaunti ya Pokot Magharibi, Stephen Kakuko, amewahimiza wahudumu wa bodaboda, ambao wanatumia barabara kuu ya Kapenguria hadi Alale kuwa makini kutokana na ongezeko la visa vya ajali.
Akizungumza moja ka moja na Aperit fm, Kakuko amewataka wahudumu hao kuzingatia sheria za uchukuzi wanapo tumia barabara hiyo akirejelea ajali iliyotokea eneo la Kitalakapel iliyohusisha pikipiki mbili ambapo mtu mmoja alipoteza maisha na wengine kujeruhiwa.
Aidha Kakuko amewahimiza wahudumu hao kutowaruhusu watoto kendesha pikipiki wakati huu wa likizo ndefu na iwapo watapatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria.