Wanafunzi 16 wamedhibitishwa kufariki dunia kwenye mkasa wa moto, katika shule ya wasichana ya Utumishi Senior Academy uko Gilgil kwenye kaunti ya Nakuru.
Kulingana na idara ya upelelezi dci na waziri wa elimu Julias Migos, wanafunzi wengine 79 wamelazwa hosipitalini. 73 wamelazwa katika hosipitali ya st Joseph, uku 6 wakilazwa katika hosipitali ya jeshi la ulinzi KDF.
Idara ya DCI inasema kwamba wanafunzi ambao wamefariki dunia kufuatia mkasa wa moto katika shule ya upili ya wasichana ya utumishi uko gilgil ni 16.
Akizungumza muda mfupi uliopita mmoja wa wazazi amesema kwamba hawakuwa wamepata taarifa zaidi kutoka kwenye usimamizi wa shule iyo kuhusia na tukio hilo.
Mmoja wa wakuu wa polisi aliyezungumza na wanahabari kuhusiana kisa hicho, amesema kwamba uchunguzi umeanzishwa mara moja ili kubainisha chanzo cha mkasa huo wa moto.
Aidha Rais William Ruto ametuma ujumbe wa kuzifariji familia ambazo wanao wamefariki dunia kwenye mkasa huo.
katika taarifa Rais Ruto ameomba kuwe na subira uchunguzi ukiendelea kuhusiana na chanzo cha mkasa huo.