Wito umetolewa kwa serikali kwa ushirikiano na wizara ya elimu kuweka mikakati kuwasaidia watoto kutoka familia maskini na mayatima wanaopaswa kujiunga na Gredi Ya Kumi .

Wadau Mbalimbali Katika Sekta Ya Elimu Wakiwemo Na Waalimu Wametaka Serikali Kuwa Na Mikakati Dhabiti Itakayowasaidia Watoto Wenye Hitaji Zaidi Katika Jamii. Mwakilishi Wa Akina Mama Kwenye Tume Ya Kitaifa Ya Walimu Katika Kaunti Ya Trans Nzoia Patricia Mellisa Amesisitizia Haja Ya Kuwepo Kwa Mipango Ya Kuwashughulikia Watoto Yatima.

Aidha Mellisa Ametumia Fursa Hio Kutoa Wito Kwa Mashirika Mbalimbali Kuungana Na Kushirikiana Ili Waweze Kuwasaidia Watoto Hasa Wanaopatikana Kwenye Mabanda Katika Kaunti Ya Trans Nzoia Kama Vile Matisi Na Kipsongo.