You are currently viewing GACHAGUA ASHTUMIWA KUFUATIA KAULI YAKE YA KUWATAKA WATALII NA WAWAKEZAJI KUTOZURU KENYA

GACHAGUA ASHTUMIWA KUFUATIA KAULI YAKE YA KUWATAKA WATALII NA WAWAKEZAJI KUTOZURU KENYA

Seneta wa Nandi, Samson  Cherargei, amemshutumu aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kufuatia wito wake wa kuwazuia watalii kutembelea kenya, akisema hatua hiyo ni hujuma dhidi ya uchumi wa taifa na inaweza kutafsiriwa kama usaliti.


‎Cherargei amesema kuwa kauli hizo zinaathiri sekta ya utalii, ambayo ni moja ya nguzo muhimu za uchumi wa kenya, na kudai kuwa zinaharibu taswira ya nchi kimataifa.

‎Ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuwa waangalifu wanapotoa matamshi kuhusu masuala ya kitaifa, akisisitiza umuhimu wa kulinda uchumi wa nchi na kuimarisha imani ya wawekezaji pamoja na watalii wanaotembelea kenya.