Muungano wa mashirika ya kutetea haki za kibinadamu na asasi za kiraia, umeomba Bunge la Kitaifa kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya mauaji kiholela, kutoweka kwa watu kwa lazima, mateso na matumizi ya nguvu kutipita kiasi yanayodaiwa kufanywa na maafisa wa polisi.
Ombi ilo limewasilishwa na Mratibu wa kitaifa wa vuguvugu la Mtetezi Francis Awino kwa niaba ya muungano huo.
Wanaharakati hao wanasema uchunguzi huo unalenga kuimarisha uwajibikaji wa polisi, kuboresha mifumo ya usimamizi wa vyombo vya usalama na kuhakikisha sheria zinazolinda haki za kikatiba za wakenya zinatekelezwa kikamilifu.
Jumanne wiki hii, wanaharakati hao walifanya maandamano ya amani hadi kwenye majengo ya Bunge la Kitaifa, ambako waliwasilisha rasmi ombi lao.

