Wizara ya afya imeonya kuwa uhaba wa damu unaoendelea kushuhudiwa katika hosipitali mbalimbali nchini unahatarisha maisha ya wagonjwa wanao itaji huduma za dharura na matibabu maalum.
Kwa mujibu wa wizara iyo, upungufu huo umeathiri zaidi ya waathiriwa wa ajali, akina mama wanaopata matatizo wakati wa kujifungua, watoto wenye upungufu wa damu pamoja na wagonjwa wanao itaji upasuaji na matibabu ya magonjwa sugu.
Wataalam wa afya wanasema damu salama ni rasilimali muhimu inayoweza kuokoa maisha, wakisisitiza kuwa uchungaji damu ni salama na hauna madhara kwa mtu mwenye afya njema.
Kutokana na hali iyo wizara ya afya imewataka wakenya wanao kidhi vigezo vya uchangiaji damu kujitokeza mara kwa mara katika vituo vya ukusanyaji damu, ili kusidia kuongeza akiba ya damu na kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanao itegemea.

