You are currently viewing VIONGOZI WA KIKE KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WATEMA MOTO

VIONGOZI WA KIKE KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WATEMA MOTO

Viongozi wa kike katika kaunti ya pokot magharibi, wameendelea kutoa hamasa kwa wakazi wa kaunti hiyo kujiandikisha kwa wingi kupata vitambulisho vya kitaifa na kujisajili kuwa wapiga kura.

Wakiongozwa na Marshana Cheruto mwakilishi wadi maalum wa wadi ya Mnagei eneo bunge la Kapenguria, na Mary Mule wa wadi ya Kapchok eneo bunge la Kacheliba katika kaunti ya Pokot Magharibi, wamewahimizi viongozi kaunti hiyo, kuzingatia matamshi wanayoyatoa kwenye hadhara ili kuzuia kuleta vurugu za mara kwa mara.

Marishana amewataka viongozi kuendelea kuhubiri amani na kuuza sera za kweli bila kejeli na malumbano, uku akisema baadhi ya viongozi katika kaunti hiyo wanatumia promaganda kutafuta umaarufu wa kisiasa.

Ameendelea kwa kusema kuwa kuna baadhi ya viongozi katika kaunti ya Pokot Magharibi, akimuhusisha mwakilishi wadi maalum Elijah Kasheusheu maarufu kama Ozil, kwa kupanga vurugu kwenye hafla za kisia.

Anasema kasheusheu amekuwa na mazoea ya kuwakodi vijana toka kaunti jirani ya Trans Nzoia eneo la Matisi, ili kutatiza shughuli za kisiasa katika kaunti ya Pokot Magharibi, akisema anausika pakubwa katika vurugu eneo la Alale kwa kumpinga aliyekuwa mbunge eneo hilo Mark Lomunokol, uku akivitaka vyombo vya habari kufanya kikao na kambi zao ili kubaini ukweli na propaganda.

Kwa upande wake Mary Mule, ameonekana kumkejeli mwakilishi wadi maalum wa Mnagei Esther Chepution, kwa kueneza propaganda dhidi ya viongozi wenzake wa kike katika kaunti ya Pokot Magharibi haswa wa mrengo wa 5G, ili kusifiwa na gavana wa Pokot Magharibi Simon Kachapin, hali inayompelekea hata kumuita gavana mungu wake.

APERIT FM, HII NI YETU