You are currently viewing WAATHIRIWA WA MAANDAMANO YA AFRIKA KUSINI, WAIOMBA MSAADA SERIKALI YA KENYA

WAATHIRIWA WA MAANDAMANO YA AFRIKA KUSINI, WAIOMBA MSAADA SERIKALI YA KENYA

Wakenya 477 waliorejea nchini kutoka Afrika Kusini mapema mwezi huu kufuatia mashambulizi ya chuki dhidi ya raia wa kigeni sasa wanaitaka serikali kuwapa msaada wa kifedha ili waanze upya maisha yao.

Wawakilishi wa waliorejea nchini walikutana na maafisa wa idara ya maswala ya wakenya wanaoishi ughaibuni, wakisema wengi wao walirejea nchini bila ajira, biashara wala chanzo cha mapato.

Kiongozi wao Baylian Wambugu, amesema wanaitaji ufadhili wa kuwasaidia kuanzisha biashara na kujikimu kimaisha, akiishukuru serikali kwa kuwaokoa nchini Afrika Kusini.

Mbali na changamoto za kiuchumi, raia hao wanasema watoto wengi waliozaliwa Afrika Kusini, hawana vyeti vya kuzaliwa vya Kenya, jambo linalo wazuia kujiunga na shule za hapa nchini.

Aidha baadhi yao walirejea bila vitambulisho vya kitaifa, uku familia nyingine zikiiomba serikali kuwasaidia kurejesha miili ya jama wao, ambao walifariki dunia Afrika Kusini.