Timu hizo sasa zitaungana na mataifa ya Taiwan, Uzbekistan, Papua New Guinea na Venezuela au Ecuador katika mashindano ya mataifa sita mwezi Novemba na Disemba na kusaka nafasi ya timu mbili.
Timu za taifa za wanawake za Afrika Kusini na Ghana zimefanikiwa kutinga katika hatua ya mchujo ya Kombe la Dunia la Wanawake 2027.
Ghana waliibamiza Ivory Coast 2-1 huku Afrika Kusini licha ya kuwa pungufu wakiwabamiza vigogo Nigeria 2-1.
Timu hizo sasa zitaungana na mataifa ya Taiwan, Uzbekistan,Papua New Guinea na Venezuela au Ecuador katika mashindano ya mataifa sita mwezi Novemba na Disemba na mbili zitakapofanya vyema zikitarajiwa kusonga mbele katika Kombe la Dunia.
Huko Morocco, Siku ya Jumamosi, Morocco itakabiliana na Algeria kwa nafasi ya tatu katika michuano ya WAFCON na, Jumapili, Malawi itakutana na Cameroon katika mchezo wa fainali. Mechi zote mbili zitachezwa mjini Rabat.
APERIT FM, HII NI YETU

