Bunge la kitaifa limepitisha katika usomaji wa pili mswada wa marekebisho ya sheria ya michezo ya mwaka 2026, hatua inayolenga kuharamisha upangaji wa matokeo ya mechi na aina nyingine za udanganyifu, katika mashindano ya michezo hapa nchini.
Mswada huo unaodhaminiwa na mbunge maalum Irene Mayaka, unapendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa kisheria wa kubainisha, kuchunguza na kuwaadhibu wanao husika na vitendo vinavyo hujumu uhadhilifu wa michezo.
Iwapo utapitishwa kuwa sheria, taasisi husika zitapewa maamlaka ya kufanya uchunguzi uku atakaye patikana na hatia akihukumiwa kifungu cha hadi mwaka mmoja gerezani, kulipa faini ya hadi shilingi milioni moja au adhabu zote mbili.
Mbunge wa Yatta Basil Ngui ni miongoni mwa wabunge waliounga mkono mswada huo.
Hata hivyo, kulingana na msada huo, Sports Kenya, itapewa jukumu la kupokea taarifa za tuhuma, kuanzisha uchunguzi na kushirikiana na vyombo vya uchunguzi wa jinai ili kukamilisha uchunguzi ndani ya kipindi kisichozidi miezi Sita.
Baada ya kupitishwa kwenye usomaji wa pili mswada huo sasa utajadiliwa katika kikao cha wabunge wote, watakao chambua kila kifungu kabla ya kupiga kura ya mwisho.

