You are currently viewing MAMA WA TAIFA RACHAEL RUTO ASISITIZA UMUHIMU WA WANAWAKE KUWEZESHWA KIUCHUMI

MAMA WA TAIFA RACHAEL RUTO ASISITIZA UMUHIMU WA WANAWAKE KUWEZESHWA KIUCHUMI

Mama wa taifa  Rachel Ruto amesema   uwezeshaji wa wanawake unapaswa kuwa endelevu  kwa misingi kwamba inawapa  wanawake ujasiri na uhuru wa kufanya maamuzi, kusaidia familia zao na kujenga maisha bora kwa siku zijazo.

Akizungumza katika eneo la Tinderet kaunti ya Nandi, Mama Rachel amesema kuwa mwanamke aliyewezeshwa huwa na uwezo mkubwa wa kushiriki katika maamuzi yanayohusu maisha yake, familia yake na jamii kwa ujumla.

Amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika fursa zinazowawezesha wanawake kujitegemea kiuchumi na kijamii, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kujenga familia na jamii imara.

APERIT FM,HII NI YETU